Serikali inashikilia kuwa shule hazitafungwa licha ya virusi vya corona kuzidi kuongezeka katika siku za hivi karibuni, ambapo walimu 33 wameambukizwa virusi hivyo.
Katibu wa wizara ya Elimu Belio Kipsang’ amewaambia wabunge kwamba wafanyakazi wanne wa shule pia wamethibitishwa kuambukizwa virusi hivyo.
Kipsang’ alieleza kuwa jumla ya shule 35 kote nchini zimenakili visa vya ugonjwa huo.
Hata hivyo, alitupilia mbali uwezekano wa shule kufungwa kutokana na hali hiyo.
Katibu huyo vile vile amewataka wazazi kulipa karo ili kuzisadia shule kuendelea na masomo pasipo kutatizika.









