Mtoto wa miezi tisa ni miongoni mwa watu 1,018 wamepatikana na virusi vya corona baada ya kupima sampuli 6,649 katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.
Waziri wa afya Mutahi Kagwe anasema hii ni inafikisha 51,851 idadi ya visa vya ugonjwa huo nchini kufikia sasa.
Nairobi imeripoti visa 199, Mombasa 117, Kiambu 102, Kericho 73, Nakuru 67 na Bungoma 66.
Idadi ya waliofariki inaendelea kupanda baada ya wagonjwa 16 zaidi kufariki na kufikisha idadi ya maafa kuwa 950.
Idadi ya waliopona imefikia 35,258 baada ya kupona kwa watu 426; 312 wakipna wakiwa nyumbani na wengine 114 wakipona wakiwa hospitalini.
Wagonjwa walio hospitalini ni 1,060, walio nyumbani ni 4,230.
Walio katika chumba cha watu mahututi ni 36, 14 wanasaidiwa na mashine kupumua.