Serikali yapiga marufuku mikutano ya kisiasa

0

Mwaka mmoja tangu Kenya kurekodi kisa cha kwanza cha virusi vya corona, Rais Uhuru Kenyatta katika hotuba kwa taifa kutoka ikulu ya Rais amesema iwapo serikali ingekosa kuchukua hatua za dharura, zaidi ya wakenya million moja wangekuwa wamemabukizwa corona na wengine elfu mia moja na hamsini kufariki.

Ni kutokana na hilo ambapo katika hotuba yake, Rais amelenga maeneo ambayo yamenonekana kupuuza masharti ya kuzuia msambao wa corona. Mikutano ya wanasiasa.

Rais ameagiza kusitishwa kwa mikutano yeyote ya kisiasa kwa muda wa siku thelathini kuanzia usiku huu.

Hii si mara ya kwanza kwa serikali kupiga marufuku mikutano ya kisisa, Novemba mwaka uliopita, serikali ilipiga marufuku mikutano ya wanasiasa kwa siku sitini, ila utekelezaji wake ukagonga mwamba.

Akionekana kulenga maafisa wakuu serikalini ambao wamekuwa wakiandaa mikutano ya kisiasa bila kufuata masharti ya kuzuia msambao wa corona, amiri jeshi mkuu ameagiza polisi kuhakikisha kuwa agizo hilo linateklezwa bila kujali hadhi ya waandalizi.

Wakati uo huo, Rais ameongeza muda wa kuendelea kutekelezwa kwa amri ya kutotoka nje kwa siku sitini zaidi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here