Ni pigo kwa wakenya baada ya tume ya kudhibiti kawi nchini EPRA kuongeza bei ya mafuta.
Katika notisi, kaimu mkurugenzi wa EPRA Daniel Kiptoo anasema kuanzia hii leo mafuta ya petrol yameongzeka kwa shilingi 7.63, diseli kwa shilingi 5.75 na mafuta taa kuongezeka kwa shilingi 5.41
Hii ina maana kuwa lita moja ya petrol jijini Nairobi inauzwa kwa shilingi 122.81 kutoka shilingi 115.81 kwa lita ambazo ilikuwa inauzwa hapo jana.
Mafuta ya diseli Nairobi sasa yanauzwa shilingi 107.66 kwa lita kutoka shilingi 101.91 kwa lita.
Familia maskini ambazo hutumia mafuta taa hasijazwa kwani lita moja ya mafuta taa Nairobi sasa ni shilingi 97.85 kutoka shilingi 92.44.
Huu ni mwezi wa tatu mfululizo tume hiyo inaongeza bei ya mafuta, ila mwezi huu, bei hizo zimepanda kwa kiwango kikubwa.
Hatua hiyo huenda ikachangia kuongezeka kwa nauli, umeme na pia bei ya bidhaa muhimu ambazo hutegemea mafuta kuzalisha.
Kiptoo anatetea hatua yao kupandisha bei akisema imetokana na kuongezeka kwa bei ya mafuta hayo katika soko la dunia.
Licha ya hayo,
Chama cha ODM kimepinga vikali hatua ya tume ya kudhibiti kawi nchini EPRA kuongeza bei ya mafuta.
Katika taarifa, katibu mkuu wa Chungwa Edwin Sifuna ameitaka EPRA kufutilia mbali bei hizo mpya akizitaja kuwa mzigo mkubwa kwa mlipa ushuru.
Sifuna anasema hatua ya serikali kutafuta ushuru zaidi kutoka kwa wakenya ambao wamelemewa na makali ya janga la covid19, ni sawa na kukamua ngombe aliyefariki.
Sifuna anasema sekta mbalimbali zitaathirika na nyongeza hiyo ikizingatiwa kuwa sekta nyingi hutegemea mafuta.