Wakenya wapinga nyongeza ya bei ya mafuta

0

Baadhi ya Wakenya wameelezea kughadhabishwa kwao na hatua ya serikali kuongeza bei ya mafuta.

Wananchi kutoka sehemu mbalimbali nchini ambao wamezungumza na Shajara wanasema hatua hiyo ni pigo kubwa kwao kwani kwa sasa wamelemewa na janga la corona ambalo limesababisha baadhi kuachishwa kazi.

Aidha wahudumu wa matatu wanasema itakuwa vigumu kupandisha nauli haswa ikizingatiwa kuwa wanabeba abiria nusu ili kufuata masharti ya kujikinga na virusi vya corona.

Kwenye bei mpya zilizotangazwa na tume ya kudhibiti kawi EPRA, mafuta ya petrol yameongzeka kwa shilingi 7.63, diseli kwa shilingi 5.75 na mafuta taa kuongezeka kwa shilingi 5.41

Hii ina maana kuwa lita moja ya petrol jijini Nairobi inauzwa kwa shilingi 122.81 kutoka shilingi 115.81 kwa lita ambazo ilikuwa inauzwa hapo jana.

Mafuta ya diseli Nairobi sasa yanauzwa shilingi 107.66 kwa lita kutoka shilingi 101.91 kwa lita.

Familia maskini ambazo hutumia mafuta taa hasijazwa kwani lita moja ya mafuta taa Nairobi sasa ni shilingi 97.85 kutoka shilingi 92.44.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here