Wakili Willis Otieno amekosoa utawala wa Kenya Kwanza kwa kile alichokitaja kama ukimya na ulaghai wa kisaikolojia kufuatia kupanda kwa bei ya mafuta hivi majuzi.
Willis ameshutumu serikali kwa kufuata mtindo unaotabirika na wa matusi ambapo inaongeza bei ya mafuta kwa kasi bila maelezo, kisha kusubiri ghadhabu ya umma kupungua kabla ya kupunguza kidogo na kuziuza kama mafanikio makubwa.
Haya yanajiri saa chache baada ya Mamlaka ya kudhibiti kawi na Petroli EPRA kutangaza kuongezeka kwa bei za mafuta katika makadirio yake ya kila mwezi ikitaja sababu ya hali hiyo kuchangiwa na kuongezeka kwa gharama za uagizaji wa mafuta kwenye daraja la kimataifa na shinikizo la ubadilishanaji wa fedha za kigeni
Kwa mujibu wa taarifa za EPRA ni kwamba bei za rejareja kutoka julai 15 hadi Agosti 14 kwa mafuta zimepanda kwa wastani wa shilingi tisa kwa kila lita
Hatua hii ina maana kuwa wakaazi hapa jijini Nairobi watanunua petrol kwa shilingi 186.31 kwa lita, dizeli kwa shilingi 171.58 na mafuta ya taa kwa shilingi 156.58 kwa kila lita
Jijini Mombasa bei ni ya chini kiasi ikilinganishwa na Kisumu ambapo wakazi watakuwa wakinunua petrol kwa shilingi 186.15 kwa lita huku mafuta ya taa yakiuzwa kwa shilling 156.83 kwa lita








