NYS YAKANA KUHUSIKA NA VURUGU ZA SABASABA

0

Huduma ya Vijana kwa Taifa (NYS) imepuuzilia mbali madai kwamba mabasi yake yalitumiwa kuwasafirisha watu walioripotiwa kuhusika katika visa vya uhalifu wakati wa maandamano ya hivi majuzi ya Saba Saba mjini Naivasha.

Katika taarifa yake, NPS imetaja ripoti kwamba wahuni walisafirishwa hadi Naivasha katika mabasi ya NYS chini ya ulinzi wa polisi kuwa za uwongo na za kupotosha, zilizokusudiwa kuchafua sifa ya taasisi hiyo.

Kamanda Jenerali wa NyS amekariri kuwa taasisi hiyo haijawahi kujihusisha na maswala ya kisiasa au shughuli zozote zisizo halali.

Amewataka wananchi, vyombo vya habari na viongozi wa kisiasa kujiepusha na kile NYS ilichoeleza kuwa ni kueneza habari ambazo hazijathibitishwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here