Komora ateuliwa mwenyekiti wa NPSC

0

Rais William Ruto amemteua Amani Yuda Komora kuwa mwenyekiti wa tume ya kitaifa ya huduma ya polisi (NPSC)

Uteuzi wake ulitangazwa kupitia gazeti rasmi la serikali siku ya Jumatatu na mkuu wa utumishi wa umma Felix Kosgei kwa mujibu wa katiba pamoja na kanuni za tume hiyo.

“Rais ametekeleza jukumu lake la kikatiba kumteua Dr. Komora kuwa mwenyekiti wa NPSC.”

Uteuzi wa Komora umefuatia kukamilika kwa muhula wa kuhudumu wa mwenyekiti wa zamani Eliud Kinuthia.

Komora aliyekua naibu mwenyekiti wa tume ya kuratibu mishahara ya wafanyikazi wa umma (SRC) pia aliwahi kuwa meneja mkuu wa wafanyikazi katika mamlaka ya bandari (KPA).

Mwingine ambaye ameteuliwa kuwa mwanachama wa NPSC ni Angeline Yiamiton Siparo, ambaye atajiunga na Peris Muthoni Kimani, Benjamin Juma Imai na Collete Suda ambao watahudumu kwa kipindi cha miaka sita iwapo wataidhinishwa na bunge la kitaifa.

NPSC huwa na majukumu muhimu ambayo pamoja na mengine ni uajiri, kuwapandisha vyeo maafisa wa polisi ndani ya huduma ya kitaifa ya polisi sawa na masuala ya kinidhamu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here