Sammy Leshore kuchukua nafasi ya Isaac Mwaura

0

Aliyekuwa seneta wa Samburu Sammy Leshore ameteuliwa kuchukua wadhifa wa Isaac Mwaura aliyefurushwa na chama cha Jubilee.

Kwenye gazeti rasmi la Mei 10, 2021, tume ya uchaguzi IEBC imechapisha jina la seneta huyo wa zamani kujaza nafasi hiyo kuwakilisha watu wenye ulemavu bungeni.

Uteuzi huu unafanywa licha ya kuwepo kwa agizo la mahakama linalozuia kuondolewa kwa Mwaura.

Jaji wa mahakama kuu ya Milimani Joseph Sergon ameratibu kesi hiyo kusikilizwa Machi 24.

Spika wa bunge la Senate Ken Lusaka litangaza kiti cha Mwaura kuwa wazi kupitia kwa gazeti rasmi la serikali kuanzia Mei 7 mwaka huu wa 2021.

Mwaura alipoteza kiti chake baada ya jopo la kutatua mizozo ya vyama vya kisiasa kuamuru kwamba chama chake cha Jubilee kilikuwa sawa kumfurusha kwa kuzingatia sheria za vyama vya kisiasa.

Jubilee ilimtimua Mwaura kwa misingi kwamba amekuwa akiuza sera za chama kingine kinyume na kanuni zinazolinda vyama vya kisiasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here