Naibu rais William Ruto ametetea utendakazi wa serikali ya Jubilee dhidi ya shutuma kwamba imefeli katika ahadi ilizotoa kwa Wakenya kipindi cha uchaguzi.
Akimjibu kinara wa chama cha ODM Raila Odinga alipoandaa mkutano wa kisiasa katika soko la Burma jijini Nairobi, Ruto amesema rekodi ya Jubilee kimaendeleo inaonekana kuanzia kwa ujenzi wa reli ya kisasa.
Ruto ambaye hotuba yake ilikatizwa baada ya kuzomewa na kundi moja la vijana vile vile amemtaka Odinga kuachana na serikali iwapo anahisi kuchoka na handisheki baina yake na rais Uhuru Kenyatta.