Mutyambai awaonya wanaboda boda dhidi ya uhuni

0

Inspekta Jenerali Hillary Mutyambai ametoa onyo kali kwa wana bodaboda wanaoendeleza uhuni wa kuwashambulia madereva wa magari.

Katika taarifa Mutyambai ameonya kuwa wahudumu wa boda boda wanaowachapa madereva na kuchoma magari yao kwa kudaiwa kuhusika katika ajali za wenzao watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Mutyambai vilevile amewataka Wakenya kuripoti visa vya utovu wa nidhamu kama hivyo vinapotokea.

Vilevile amewaagiza maafisa wa Polisi kuanzisha msako dhidi ya wahudumu wa boda boda wanaokiuka sheria za trafiki.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here