Naibu rais William Ruto amewataka Polisi kuwakamata na kuwashtaki waliohusika na na rabsha za Jumapili katika eneo la Kenol kaunti ya Muranga ambapo watu wawili waliuawa.
Ruto anasema waliohusika na kupanga vurugu hizo ni watu wanaojulikana.
Naibu rais amedai kuwa rabsha hizo za Murang’a ilikuwa ni maendelezo ya kilichotendeka Kisii mwezi mmoja uliopita ambapo amesema vijana walitumwa kuvuruga mkutano wake.
Akizungumza alipokutana na viongozi kutoka kaunti ya Narok katika afisi zake Karen, Ruto amesema wakuu wa mikoa wamekuwa wakitumika kutatiza mikutano yake.









