Watu 22 wamepatikana na virusi vya corona baada ya kupima sampuli 595 katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita na kufikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa 39,449.
Katibu katika wizara ya afya Dkt. Rashid Aman ameripoti kufariki kwa watu 4 zaidi na kufikisha idadi ya maafa kuwa 731.
Idadi ya waliopona imefika 27,035 baada ya watu wengine 376 kupona kutokana na ugonjwa huo.
Msambao wa virusi hivi ni kama ifuatavyo; Nairobi 18, Meru 2 Nakuru & Kiambu 1.