Seneta wa Makueni Mutula Kilonzo Junior ameorodheshwa kuwa wa kwanza kwa utendakazi ikilinganishwa na maseneta wenzake.
Kwa mujibu wa utafiti wa shirika la Infotrak, seneta Kilonzo amepata asilimia 66.4 ya utendakazi akifuatwa na mwenzake wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen aliyepata asilimia 58.8.
Walter Nyakundi ni meneja wa utafiti katika kampuni hiyo.
Maseneta waliovuta mkia ni Golich Wario (Tana River), Abdullahi Ibrahim (Garissa), Mwangi Githomi (Nyandarua), Michael Mbito (Trans Nzoia) na Amos Wako (Busia).
Mkurugenzi mkuu wa Infotrak Angela Ambitho anasema matokeo ya utafiti huo ni baada yao kuwahoji wananchi ambao walipewa fursa ya kuwapa alama maseneta wao.
Utafiti huo umewaorodhesha maMCA Makueni na Embu kuwa wachapa kazi zaidi kwa asilimia 54.2% wakifuatwa na wale wa Baringo na Vihiga ambao wameapata asilimia 54.2%.
Bunge la kaunti ya Makueni limetajwa kuwa la kwanza katika kuwajibikia majukumu yake kwa asilimia 58.5% likifuatwa na bunge la Kwale na Pokot Magharibi.









