BBI imeturusha nje wateta viongozi wa kidini

0

Viongozi wa makanisa sasa wanasema maoni yao yalipuuzwa kwenye ripoti ya mwisho ya BBI.

Viongozi wa muungano wa makanisa ya kievangelisti wakiongozwa na kasisi Mark Kariuki wanasema miongoni mwa maoni waliyotoa na kupuuzwa ni pendekezo la kuteua mwakilishi wa kanisa katika ngazi ya kaunti.

Maaskofu hao akiwemo Stephen Mutua wanataka ripoti hiyo kufanyiwa marekebisho ili kujumuisha kila mkenya.

Aidha, wamekosoa kuhusishwa kwa wanasiasa katika maswala ya tume ya uchaguzi IEBC na kuitisha mkutano mwingine wa kitaifa ili maswala ibuka yajadiliwe.

Hayo yakijiri

Naibu rais William Ruto ameonya dhidi ya kuugeuza mjadala wa BBI na kuwa swala baina ya rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga.

Badala yake Ruto ameendelea kushinikiza kuwepo kwa mchakato utakaohakikisha kuwa kunakuwa na makubaliano ya pamoja pasipo kuwa na wanaopinga na wanaounga mkono.

Kupitia mtandao wake Twitter, Ruto amesema hilo litaafikiwa kupitia kujumuisha maoni ya wale wanaohisi kusahaulika.

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here