Rais Ruto Ataka Tume ya Kukabili Ufisadi EACC Kuwakamata Wafisadi.

0

Rais William Ruto sasa ameitaka Tume ya Maadili na kukabiliana na ufisadi (EACC) kufanya jukumu lake la kuwakamata wote wanaojihusisha na maswala ya ufisadi katika serikali yake.

Akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa kongamano la tisa la ugatuzi kwenye kaunti ya Homabay, Rais ameunga mkono kauli ya spika wa bunge la seneti Amason Kingi kuwa magavana waliopatikana wakijihusisha na ufisadi wachukuliwe hatua kali za kisheria.

Rais aidha ameongeza kuwa pia wabunge wanapaswa kuwajibika iwapo watahusika na maswala ya ufisadi.

Pia ameitaka idara ya mahakama kushughulikia maswala ya ufisadi kwa njia ifaayo.

Aidha amezitaka serikali za kaunti kutumia mgao wake wa fedha kufanikisha maendeleo na kubadilisha maisha ya wakenya akisisitiza kuwa mgao wa shilingi bilioni 415 kwenye mwaka wa kifedha wa 2025/2026 unalenga kuziwezesha serikali za kaunti hata Zaidi.

Kiongozi wa taifa amesisitiza kujitolea kwa serikali yake kufanikisha usambazaji wa fedha za kaunti kwa wakati.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here