RAIS RUTO ADOKEZA KUWA NA NAIBU MWANAMKE KATIKA UCHAGUZI UJAO

0

Huenda muungano wa Kenya Kwanza ukawa na mwaniaji mwenza wa Urais wa jinsia ya Kike katika chaguzi zijazo amedokeza Rais William Ruto.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa muungano wa Magavana wanawake almaarufu G7, Rais Ruto amesema wanaanda majadiliano na naibu wake Rigathi kufanikisha hilo akirai magavana sawia kuwa na manaibu wa jinsia tofauti.

Rais amemjukumisha Gavana wa Kaunti ya Embu Cecily Mbarire amabye ni mwenyekiti wa Chama Tawala cha UDA kubuni sera itakayohakikisha kuwa anaepeperusha bendera ya chama hicho katika kinyanganyiro cha urais anateua naibu wa jinsia tofauti.

“Kuenda mbele mimi na Riggy G tutaketi chini na kukubaliana kwamba iwepo mwaniaji wa chama cha UDA ni mwanaume mwaniaji mwenza anakuwa mwanamke akiwa mwanamke naibu wake anakuwa mwanaume. ” Rais alisema.

“Najua kinara wa wiper alimuunga mkono Wavinya Ndeti, Gavana Wanga sawia aliunga mkono na kinara wa chama chake. Tunafanya hili kimaksudi kuhakikisha kuwa tunatimiza hitaji la thuluthi ya jinsia.” Aliongereza Rais.

Rais aidha amerai wanaume kuwa kwenye mstaari wa mbele kutetea haki za wanawake na kuwalinda dhidi ya ukeketaji ambao amesema umepitwa na wakati.

“ Ukeketaji unaharibu wanawake. Unawafanya wanawake kutojiamini na kupunguza uwezo wao wa kutimiza majukumu yao ya kike.” Amesema Rais.

Muungano wa G7 unaleta pamoja magava wote saba waliochaguliwa katika uchaguzi kuu uliopita na unadhamiria kuunga mkono juhudi za wanawake katika uongozi hususan kwenye ngazi ya kaunti.

Magavana hao wanajumuisha Ann Waiguru(Kirinyaga), Gladys Wanga(Homa Bay), Susan Kihika(Nakuru), Wavinya Ndeti(Machakos), Fatuma Achani(Kwale), Kawira Mwangaza(Meru) and Cecily Mbarire(Embu).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here