FAMILIA YAPONEA MLIPUKO WA GESI EMBAKASI

0
NAIROBI GAS FIRE

Familia moja kutoka eneo la Embakasi kaunti ya Nairobi imeponea chupuchupu baada ya gesi iliyokuwa inatumika kupikia kulipuka usiku wa kuamkia leo.

Kulingana na ripoti ya polisi hakuna amabye amejeruhiwa kati ya familia hiyo ya watu watatu ila moto kutokana na mlipuko umeharibu sehemu ya nyumba yao.

Familia hiyo immetaja kwamba walikuwa kwenye harakati za kuandaa chakula wakati mtungi wa gesi waliokuwa wanatumia ulilipuka.

Polisi wameanza uchunguzi wa kisa hicho ambacho na cha hivi karibuni kwa kuhusisha mlipuko wa gesi.

Mwezi uliopita, angalau watu watatu wa familia moja walipata majeraha wakati gesi ililipuka nyumbani kwao eneo la Kayole hapa hapa Nairobi.

Watatu hao walijumuisha watoto wa miaka tata, nane na 15.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here