Raila Odinga asema BBI bado iko

0

Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga ameelezea matumaini yake kwamba mchakato wa kubadilisha katiba kupitia BBI utaendelea licha ya kutiwa breki na mahakama.

Akiwahutubia mamia ya wafuasi wake waliojitokeza kumkaribisha mjini Kisumu, Odinga amewataka Wakenya kutokuwa na wasiwasi kuhusu ubadilishaji wa katiba hata kama mahakama imesimamisha mchakato huo.

Waziri huyo mkuu wa zamani ambaye yuko Kisumu kukagua maandalizi ya sherehe za Madaraka alikutana faraghani na viongozi wa kisiasa kutoka kaunti hiyo.

Aliwaambia kwamba wamewatafuta mawakili wenye tajriba kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo wa mahakama kuu.

Seneta wa Siaya James Orengo pamoja na mbunge wa Rarieda Otiende Amollo ni miongoni mwa mawakili wataokuwa kwenye kundi hilo la mawakili.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here