Martha Koome akabidhiwa rasmi majukumu ya Jaji Mkuu

0

Jaji mkuu Martha Koome amekabidhiwa rasmi mamlaka huku akiahidi kupambana na mrundiko wa kesi mahakamani.

Ili kuafikia lengo hilo, Koome ambaye ni mwanamke wa kwanza kushikilia wadhifa huo amesema atashirikiana na wenzake katika idara ya mahakama kuhakikisha kwamba haki imepatikana kwa haraka.

Akimkabidhi Koome mamlaka baada ya kushikilia wadhifa huo kwa muda, naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu ameahidi ushirikiano ili kuhakiksiha kwamba idara ya mahakama inawajibikia vilivyo majukumu yake.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Jaji Mkuu mstaafu David Maraga aliyemshauri Koome kumuweka Mungu mbele wakati wowote.

Koome amekabidhiwa katiba ya mwaka 2010 na bendera ya mahakama na ripoti ya idara ya mahakama.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here