Polisi kupambana na wachochezi wakati wa uchaguzi asema Matiang’i

0

Kuanzia wiki ijayo, idara ya polisi itaanza kutambua maeneo ambayo huenda vurugu za uchaguzi zikatokea ili kuweka mikakati ya kudumisha amani.

Akizungumza katika kongamano la inspekta mkuu Hillary Mutyambai na makamanda wa polisi kutoka kote nchini, Waziri wa Usalama wa ndani Dr Fred Matiangi amesema hawataruhusu mtu yeyote kuvuruga amani ya Kenya.

Matiangi amewataka makamanda hao kutotishwa na wanasiasa na kuruhusu visa ambavyo vinaweza kusababisha machafuko nchini.

Haya yanajiri siku moja tu baada ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma Noordin Haji kusema taifa linakosa sheria madhubuti za kuwashtaki wanaosababisha vurugu haswa wakati wa uchaguzi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here