Koome kuongoza kikao cha kwanza cha mahakama ya upeo Jumanne

0

Jaji Mkuu Martha Koome ataongoza kikao chake cha kwanza katika mahakama ya upeo hapo Jumanne hii.

Mahakama ya upeo ambayo kwa sasa iko na majaji wote kufuatia kuteuliwa kwa jaji William Ouko inatazamiwa kusikiliza kesi 20 kati ya Julai na Octoba mwaka huu wa 2021.

Kesi ya hukumu ya kifo maarufu kama Muruatetu itashughulikiwa na mahakama hiyo ya juu zaidi nchini.

Mahojiano ya kumtafuta mrithi wa David Maraga yaliangazia pakubwa kesi hiyo ya Muruatetu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here