Mamlaka inayosimamia Nairobi (NMS) limehairisha majaribio ya tatu kwenye stendi ya matatu ya Green Park yaliyokuwa yafanyike Jumatano.
Katifa taarifa, NMS imesema hatua hiyo itahakikisha kuwa umma umepata ufahamu vizuri kuhusu majaribio hayo ili washiriki kikamilifu.
Majaribio hayo yalikuwa yanatazamiwa kuendeshwa kati ya saa kumi na mbili na saa mbili asubuhi.
Matatu yaliyokuwa yashirikishwe ni yale yanayohudumu kwenye barabara za Langata, Ngong, Rongai, Kibra, Kawangware, Kikuyu, Highrise, Ngumo, Kiserian, Otiende, Madaraka na Nairobi West.