Naibu Gavana wa Kisii Joash Maangi anusurika kifo, gari lake likichomwa

0

Naibu gavana wa Kisii Joash Maangi amenusurika kifo huku gari lake likichomwa baada ya kuhusika kwenye ajali katika eneo la Olulung’a katika barabara ya Narok-Bomet na kuwaua watu wawili akiwemo mhudumu wa boda boda.

Ripoti ya Polisi inaonesha kuwa ajali hiyo ilitokea mwendo wa saa kumi na mbili na nusu wakati gari la Maangi aina ya Prado lilimgonga mwendesha boda boda John Sanyo aliyekuwa amembeba mwanawe mwenye umri wa miaka minane na kuwaua papo hapo.

Maangi pamoja na dereva wake Stanley Gitonga waliokuwa wanatoka Bomet kuelekea Narok walilazimika kutorokea maisha yao kwani vijana waliojawa na ghadhabu walichukua hatua ya kuchoma gari lao huku wakitaka kuwaadhibu kufuatia ajali hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here