Kaunti ya Kajiado yapitisha BBI

0

Bunge la kaunti ya Kajiado limekuwa la SABA kupitisha mswada wa marekebisho ya katiba BBI.

Kajiado inajiunga na Trans Nzoia, Pokot Magharibi, Busia, Homa Bay, Kisumu na Siaya kupitisha mswada huo.

Hii inamaanisha kwamba mswada huo unahitaji kuungwa mkono na kaunti 17 pekee ili kuwasilishwa bungeni na kisha kura ya maamuzi.

Kufikia sasa, bunge la kaunti ya Baringo ndilo la kipekee kupinga mswada huo.

Mswada huo unahitaji kuungwa mkono na mabunge ya kaunti yapatayo 24 kati ya 47 ili kufanikisha mabadiliko ya sheria.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here