Mwanamke aliyeibia mwanamume mmoja Sh1.6M aachiliwa kwa dhamana

0

Mwanamke anayedaiwa kumuibia mwanamume mmoja Sh1.6M baada ya kumzuibasha ameachiliwa kwa dhamana ya Sh1M.

Beatrice Mueni Mbiu ameshtakiwa katika mahakama ya Shanzu mjini Mombasa kwa kumuibia Richard Nyasamba Wanyonyi.

Mwanamke huyo amekanusha mashtaka dhidi yake mbele ya hakimu mkaazi Yusuf Shikanda ambapo ameachiliwa kwa dhamana ya Sh1M pesa taslimu au bondi ya Sh3M.

Mueni anadaiwa kumuwekea Wanyonyi kileo walipokuwa wanajiburudisha huko Nyali na kisha kumuibia pesa zake mnamo Septemba 8, 2020.

Mshtakiwa anakabiliwa na mashtaka mengine ya kumuibia Wanyonyi Sh1.5M kutoka kwa akaunti yake ya benki pamoja na simu inayogharimu Sh30,000.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here