Sahihi za BBI zafikia 1.5M

0

Zaidi ya Wakenya milioni moja nukta tano wametia saini zao kwenye mswada wa BBI siku nne baada ya kuzinduliwa kwa zoezi hilo la kutafuta sahihi.

Makatibu wenza wa kamati ya BBI ambao ni mbunge wa zamani Dennis Waweru na mwenzake wa Suna Mashariki Junet Mohammed wameelezea matumaini yao kwamba sahihi milioni nne zitapatikana kufikia mwishoni mwa juma hili.

Haya yanajiri huku viongozi mbalimbali akiwemo Musalia Mudavadi wa chama cha Amani National Congress (ANC) Musalia Mudavadi wakiongoza zoezi la kusanya sahihi za mswada huo katika kaunti ya Nairobi na maeneo mengine nchini.

Matamshi yake yameungwa mkono na mwakilishi wa wanawake kaunti ya Vihiga Beatrice Adagala ambaye amewataka wakenya pia kuunga mkono mswada huo.

Nao Baadhi ya viongozi wa makanisa kutoka kaunti ya Nakuru wametaganza hadharani kuunga mkono mswada wa marekebisho ya katiba kupitia mchakato wa BBI licha ya wenzao kupinga.

Wakiongea baada ya kutia saini zao kwenye mswada huo, viongozi hao wamesema baadhi ya vipengee vitawafaidi haswa vijana na wakenya wote kwa ujumla, na wanataka wenzao kuunga mkono.

Kimsingi, mchakato wowote wa kubadilisha katiba unapaswa kupata sahihi milioni moja za wapiga kura ambazo ni sharti zikaguliwe na tume ya uchaguzi IEBC.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here