Mwanahabari Lorna Irungu Macharia afariki kutokana na ugonjwa wa corona.

0

Aliyekuwa mtangazaji wa kituo cha Nation FM Lorna Irungu Macharia amefariki kutokana na ugonjwa wa corona.

Lorna ambaye alikua mkurugenzi msimamizi wa kampuni ya mawasiliano ya Gina Din amekuwa akipambana na ugonjwa wa figo na atakumbukwa na wengi kwenye kipindi cha Omo-Pick-a-box kilichokuwa maarufu miaka ya tisini.

Itakumbukwa kwamba tasnia ya uanahabari wiki jana ilipoteza wenzetu wawili waliofariki kutokana na ugonjwa wa COVID19.

Robin Njogu wa shirika la Royal Media Services pamoja na Winnie Mukami wa NTV walifariki baada ya kuugua ugonjwa huo.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here