Mvutano kuhusu Mfumo Mpya wa Ununuzi Watishia Kusambaratisha Huduma

0

Mvutano kuhusu mfumo mpya wa ununuzi wa kidijitali kwenye sekta ya umma wa E-GPS unatishia kusambaratisha huduma kwenye taasisi na mashirika mbalimbali ya umma

Mfumo huo unaoshinikizwa na serikali kupitia wizara ya fedha unakabiliwa na pingamizi kali kutoka kwa wabunge na magavana wakidai kuwepo kwa mianya ya kisheria katika kuufanikisha

Licha ya pingamizi hizi na magavana kudai kwamba mfumo huo haufanyi kazi, waziri wa fedha John Mbadi amesisitiza kuwa mfumo huo unalenga kukabili ufisadi na kuhakikisha kuwapo kwa uwazi katika matumizi ya fedha za umma

Akizungumza mbele ya kamati ya utekelezaji wa katiba ya bunge Mbadi ameshikilia kwamba mfumo huo utatekelezwa huku akiwahimiza wanaoshikilia ofisi za umma kuukumbatia

Hata hivyo wanachama wa kamati hiyo waliibua maswali chungu nzima kuhusu ufaafu wa mfumo huo baadhi wakisema kwamba japo taasisi nyingi za umma zitaukumbatia sheria pia inawaruhusu kutumia mfumo wa zamani katika ununuzi wa bidhaa na huduma nyingine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here