MURKOMEN ATAKA FIDIA KUTOKA KWA CHERARGEI KWA KUMHARIBIA JINA

0

Waziri wa Barabara na Uchukuzi Kipchumba Murkomen ameelekea mahakamani kumshatiki seneta wa kaunti ya Nandi Samson Cherargei kwa kumharibia jina.

Waziri Murkomen anadai kuwa matamshi ya seneta huy okatika kikao na wanahabari mwaka jana kuwa alipokea kima cha Ksh. Bilioni 13 kupendelea kampuni ya kichina ya Wu Yi imemchafulia jina na kumshushia hadhi machoni pawakenya.

Cherargei alidaikuwa waziri Murkomen alikabidhiwa Zaidi ya shilingi bilioni moja ikiwa ni sehemu ya hongo ya shilingi bilio13 fedha ambazo waziri huyo ameficha nchini Dubai.

Waziri huyo ameiambia mahakama kuwa licha ya kumwandikia barua Cherargei akitaka amuombe radhi seneta huyo amepuuzilia mbali ombi lake.

Murkomen anataka mahakama ishurtishe Cherargei kumlipa fidia kwa kumharibia jina, kumuomba msamaha hadharani, kuchapisha msamaha hio kwenye gazeti mbili za kitaifa na kulipia gharama ya kesi hio.

Wawili hao wamekuwa wakilumbana Cherargei akimkashifu sWaziri Murkomen kwa kuendleeza ufisadi katika wizara yake.

Si mara ya kwanza Cherargei kujipata pabaya na mawaziri mazjuzi alionekana kulambana na waziri wa michezo anbabu namwamba kwa kile alidai ni kutosimamia vyema wanaridhia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here