RAIS RUTO ATIA SAINI USHURU WA NYUMBA KUWA SHERIA

0

 

Rais William Ruto ametia saini mswaada wa marekebisho ya sheria ya ujenzi wa Nyumba za bei nafuu iliyopitishwa na mabunge yote mawili na kuidhinisha utekelezwaji wake.

 Hii ina maana kwamba wakenya wataanza kukatwa asilimia 1.5 ya mishahara yao kuanzia mwisho wa mwezi huu wa Machi ili kufadhili ujenzi wa nyumba za bei nafuu.

Akizungumza wakati ilitia saini mswada huo kuwa sharia katika Ikulu ya Nairobi, Rais Ruto amesema kuwa watakaofaidika pakubwa na sharia hiyo haswa ni wakenya walio na kipato cha chini kwani watapata nafasi sawia na wale wa kipato cha juu katika kumiliki nyumba na kuwa na makazi.

“Bodaboda na mama mboga wako katika hesabu yetu. Mpango huu utamfaidi mama mboga ambaye kwa sasa kodi ya shilingi elfu tatu, kulipa shilingi elfu tatu na kumiliki nyumba. Utatoa nafasi kwa mwana bodaboda ambaye anaishi katika nyumba isiyokuwa na maji wala umeme kumiliki nyumba,” Rais amesema.

Kiongozi wa taifa amesisitiza kwamba ataendelea kuzingatia ahadi yake jinsi ilivyoainishwa katika manifesto ya serikali ya Kenya kwanza katika kuwawajibikia wananchi.

Kwa upande wake Waziri wa Ardhi Alice Wahome amesifia kutiwa saini kwa mswada huo akimsifia Rais kwa kutokata tamaa licha ya uamuzi wa mahakama wa hapo awali kusitisha utekelezwaji wake sawia na pingamizi kutoka kwa upande wa Upinzani.

Rais Ruto aidha ameishukuru mahakama Kurusu kufanyiwa marekebisho mswaada wa Nyumba ambao hatimaye ulifanyiwa marekebisho muhimu ya sheria ili kuwaruhusu wale walio katika sekta isiyo rasmi kutozwa kodi ya asilimia 1.5.

Rais Ruto atia saini Ikuluni/ State House

Kwa mujibu wa Rais Ruto, mpango wa Ujenzi wa Nyumba za bei Nafuu utatoa nafasi ya ajira kwa vijana 300,000 kufikia mwaka ujao jinsi ilivyoshuhudiwa na mmoja wa wale waliohudhuria hafla ya kutiwa saini kwa mswaada.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here