ELIJAH OBEBO APENDEKEZWA KUWA NAIBU GAVANA WA KISII

0

Gavana wa Kaunti ya Kisii Paul Simba Arati amempendekeza Elijah Obebo kuteuliwa kama Naibu Gavana baada ya kutimuliwa kwa Dr. Richard Monda. 

Obebo kwa sasa anahudumu kama mwenyekiti wa bodi ya uajiri wa kaunti hio.

Wakizungumza baada ya kupokea jina la Naibu Gavana Mteule wawakilishi wadi wakiongozwa na Kiongozi wa wengi Henry Mulaja wamesifia Obebo wakihoji kuwa anastakabadhi na tajriba hitajika kujaza nafasi hio.

“Tulimpiga msasa wakati alipoteuliwa kama mwenyekiti wa Bodi. Tunaamini anastakabadhi na tajriba.” Amesema Mulaja.

Licha ya Monda kuelekea mahakamani hapo jana kupinga kutimuliwa kwake na seneti Mulaja amesema wataendelea na mchakato wa kumpiga msasa obebo kwani hawajapokea notisi kutoka mahakama kuwa Monda amekata Rufaa

“Hatujapata agizo la mahakama kwaekataa Rufaa. Tutaendelea na mchakato wa kusaili Naibu Gavana Mteule.  Tutasimamisha shughuli ya usaili Iwapo tutapata agizo hilo.” Amefafanua Mulaja.

Monda alitimuliwa baada ya kudaiwa kutisha hongo ili kusaidia jamaa mmoja kuajiriwa katika kampuni ya usambazaji maji ya Gusii.

 

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here