Takriban wabunge 110 wametia saini hoja ya kumbandua waziri wa Ukulima Mithika Linturi.
Mbunge wa Bumula Jack Wamboka anaefadhili hoja hio tayari amewasilisha stakabadhi za mswaada huo kwa afisi ya spika akidokeza imepata uungwaji mkono wa upande wa wachache na wengi.
Kulingana na Wamboka, Linturi hafai kuendelea kushikilia wadhifa huo kutokana na Kashfa ya mbolea ghushi.
Mswaada huo unapaswa kuungwa mkono na thuluthi mbili ya wabunge ili kupitishwa.