NTSA ITAKUTIA MBARONI IWAPO HAUTATUMIA DARAJA LA KUVUKIA BARABARANI

0
AFISA WA TRAFIKI ADUMISHA USALAMA BARABARANI
AFISA WA TRAFIKI ADUMISHA USALAMA BARABARANI

Mamlaka ya Uchukuzi na Usalama Barabarani(N.T.S.A) imetahadharisha wakenya hasa wanaoetembea kwa miguu dhidi ya kuvunja sheria za trafiki. 

Kupitia akaunti yao ya mtandao wa X, NTSA imesema wanaotembea kwa miguu wanapaswa kutumia vivukio na daraja za kuvukia ipasavyo hususan katika barabara zilizonashughuli nyingi.

“Ni lazima watembea kwa miguu watumie madaraja ya miguu, njia za kupita na sehemu nyingine zilizoteuliwa ili kuhakikisha usalama wao.”NTSA imesema.

Onyo hilo  limetowela kufuatia kutiwa mbaroni kwa makumi ya wenyeji wa Nairobi waliovuka barabra ya Mombasa katika mzunguko wa Nyayo pasi na kutumia daraja la kuvukia.

“Asubuhi ya leo, watembea kwa miguu kadhaa ambao walikosa kutii sheria za trafiki walizuiliwa. ”

“Ili kuepusha usumbufu wowote, tunawahimiza watembea kwa miguu kuzingatia sheria za trafiki.”

Mamlaka hio inaendesha oparesheni ya kushurutisha umaa kutii sharia za barabarani.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here