Rais William Ruto usiku wa kuamkia leo amehutubia wakenya wanaoishi katika taifa la Ghana wakati wa tafrija speheli iliyoandaliwa kwa minajjili yake.
Mkuu wa Nchi aliandamana na Waziri wa Mahusiano ya Kigeni Musalia Mudavadi na Katibu wa Idara ya Diaspora Roseline Njogu katika mkutano huo uliondaliwa mjini Accra Ghana.
Katika ziara yake ya Ghana, Mkuu wa Nchi atafanya mazungumzo na Rais Nana Akufo-Addo wa Ghana akilenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia, kibiashara na kihistoria kati ya Kenya na Ghana.
Msemaji wa Ikulu Hussein Mohammed amedokeza kwamba katika ziara hiyo, Rais Ruto atasisitiza umuhimu wa juhudi za ushirikiano ili kuimarisha demokrasia barani afrika.
Rais Ruto makao makuu ya shirika la Eneo Huru la Biashara la Bara la Afrika (AfCFTA) mjini Accra, akilenga kutafutia soko chai na ngozi ya Kenya nchini Ghana.
Rais anatarajiwa kuzuru taifa la Guinea Bissau kwa ziara rasmi.