Mtoto wa siku saba apatikana na virusi vya corona

0

Mtoto wa siku saba ni miongoni mwa watu 981 walikutwa na virusi vya corona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita kati ya sampuli 7,529 zilizopimwa.

Hii inafikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa 148,128 huku idadi ya waliopona ikiongezeka na kufikia 100,245 baada ya kupona kwa watu wengine 665.

Wagonjwa 26 zaidi wamefariki kutokana na ugonjwa huo wa corona na kufikisha idadi ya maafa nchini kuwa 2,420, 1,172 kati yao wakiwa watu wenye umri wa miaka 60 na zaidi.

Idadi ya visa hivyo inaongezeka wakati ambapo baraza la magavana linaonya kwamba maambukizi katika jamii yanazidi kuongezeka kwenye kaunti zingine mbalimbali na Nairobi, Machakos, Kiambu, Nakuru na Kajiado ambazo zilifungwa kwa sababu ya kuendelea kuripoti msambao mkubwa.

Mwenyekiti wa kamati ya afya ya baraza la magavana ambaye pia ni gavana wa Kisumu Profesa Anyang’ Nyong’o amesema serikali za kaunti zitajitahidi kahakikisha masharti ya wizara ya afya ya kukabiliana na maambukizi hayo yanafuatwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here