Jamaa aliyelipa mahari kwa mtoto,16, Lang’ata ashtakiwa

0

Jamaa aliyemlipia mahari msichana mwenye umri wa miaka 16 ameshtakiwa katika mahakama ya Kibera.

Raphael Lekinunit amekanusha mashtaka mbele ya Hakimu Charles Mwaniki.

Stakabadhi za mahakama zinaonesha kuwa mshukiwa amekuwa akiishi na msichana huyo kama mkewe katika eneo la Hardy, Langa’ta.

Polisi walimshika baada ya kufahamishwa na jirani aliyeona wawili hao wakiishi kwa muda.

Mshukiwa aliiambia mahakama kwamba alikuwa amelipa mahari kwa msichana huyo ambayo wazazi wake hawajashikwa.

Aliiambia mahakama asimpe adhabu kali kwa sababu hana uwezo wa kupata hata Sh100.

Mahakama hata hivyo ilimuwachiliwa kwa bondi ya Sh300,000.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here