Msambweni: Wawaniaji watakaomenyana kwa uchaguzi mdogo waidhinishwa

0

Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini (IEBC) imewaidhinisha wawaniaji zaidi ya tano watakaomenyana katika kinyanganyiro cha kuwania kiti cha ubunge cha Msambweni Disemba 15.

Omar Boga wa ODM na Sheikh Mahmoud wamepata idhini hiyo baada ya kuwasilisha stakabadhi zao kwa maafisa wa tume ya IEBC.

Naibu kiongozi wa chama hicho aliyepia gavana wa Mombasa Hassan Joho na seneta wa Siaya James Orengo waliandamana na Boga kupokea idhini ya IEBC kushiriki kwenye uchaguzi huo mdogo utakaoandaliwa Disemba 15.

Wengine walioidhinishwa ni wawaniaji huru Charles Bilali, Mansury Kumaka, Hassan Mwakulonda wa chama cha Economic Democracy na Marere Wamwachai wa National Vision Party.

Haya yanajiri siku moja baada ya muwaniaji huru Feisal Bader kuidhinishwa na kuanza kampeini za kujipigia debe akiungwa mkono na wendani wa naibu rais William Ruto.

Kiti hicho kilisalia wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa eneo hilo Suleiman Dori.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here