Kaimu mkurugenzi mkuu katika wizara ya afya Dr. Patrick Amoth amekuwa Mkenya wa kwanza kupewa chanjo dhidi ya ugonjwa wa corona katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta (KNH).
Chanjo hiyo imeanza kutolewa rasmi hii leo baada ya kuwasili nchini wiki hii huku wahudumu wa afya wakipewa kipau mbele.
Afisa mkuu mtendaji wa KNH Dr. Evanson Kamuri amekuwa mkenya wa pili kupata chanjo hiyo.
Mwakilishi wa shirika la afya duniani WHO tawi la Kenya Dr. Rudi Eggers amesema kuwa chanjo hiyo ya AstraZeneca ni salama na haina madhara kiafya.
Wizara ya afya inasema zaidi ya wahudumu wa afya wapatao 400,000 kote nchini pamoja na wafanyikazi wa umma wanaotoa huduma muhimu ndio watakaopewa kipau mbele katika awamu ya kwanza ya chanjo hiyo.