Jisalimishe au tukutafute, Polisi wamwambia Echesa

0

Polisi wamemtaka aliyekuwa waziri wa Michezo Rashid Echesa kujisalimisha kwa Polisi la sivyo watamchukulia kuwa mhalifu sugu aliyejihami.

Inspekta mkuu wa Polisi Hillary Mutyambai amemuagiza Echesa kujisalimisha katika kituo chochote cha Polisi kilicho karibu kufikia saa saba Ijumaa.

Echesa amekuwa mafichoni kuanzia jana aliponaswa kwenye kamera akimchapa kofi afisa wa tume ya uchaguzi IEBC kwenye uchaguzi mdogo wa Matungu.

Mutyambai katika taarifa amesema wamekuwa wakifatilia kwa karibu uhuni ambao umekuwa ukiendelezwa na baadhi ya wanasiasa haswaa katika chaguzi ndogo vurumai anazosema hazitakubalika.

Ameonya kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaopatikana wakizua vurumai huku akiitaka bodi inayosimia utoaji leseni kwa wanaomilikia bunduki kutwaa silaha za viongozi wanaotumia visivyo bunduki zao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here