Mfichuzi wa taarifa za Covid millionaires

0

Mfichuzi wa taarifa kuhusu madai ya kupotea kwa pesa za kupambana na COVID19 Godwins Agutu, dereva wake Alex Mutuku pamoja na msaidizi wake wa kibinafsi Ken Kimathi wameachiliwa kwa dhamana ya Sh100, 000 baada ya kushtakiwa kwa ulaghai.

Agutu ambaye ni afisa mkuu mtendaji wa shirika la Network Action Against Corruption (NAAC) pamoja na wenzake wameachiliwa na hakimu mkaazi David Ndungi.

Washukiwa walikamatwa na kushtakiwa kwa tuhuma za kujaribu kumlaghai mfanyibiashara mmoja wakijifanya kuwa maafisa kutoka mamlaka ya kukusanya ushuru KRA.

Hata hivyo walikana mashtaka dhidi yao mbele ya hakimu Ndungi.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here