Maafa ya corona Kenya yafikia 725

0

Maafa yanayotokana na ugonjwa wa corona yamefikia 725 baada ya watu 7 zaidi kufariki katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe katika taarifa amesema watu wengine 210 wamepatikana na ugonjwa huo baada ya kupima sampuli 3,065 na hivyo kufikisha idadi ya visa hivyo nchini kuwa 38,923.

Idadi ya waliopona imefikia 26,114 baada ya kupona kwa watu 91 zaidi katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Nakuru inaongoza kwa kuandikisha 75, Nairobi 37, Mombasa 15, Trans Nzoia 13, Kakamega 11, Kilifi & Uasin Gishu 8, Kisumu, Machakos & Kiambu 7, Bungoma 5, Kisii 3, Elgeyo Marakwet & Nandi 2, Taita Taveta, Kajiado, Meru, Murang’a, Kericho, Baringo, Laikipia, Embu, Vihiga na Narok kisa kimoja kila mmoja.   

Jijini Nairobi, visa 37 vinatoka Westlands, Dagoreti North & Langata 5, Embakasi East & Starehe 3, Embakasi Central, Embakasi South & Kibra visa viwili kila mmoja.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here