Maambukizi ya corona nchini yafikia 39, 427

0

Kenya imerekodi visa 243 zaidi vya corona baada ya sampuli 4, 385 kupimwa na kufikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa 39, 427.

Katika taarifa, wizara ya afya inasema mtoto wa miezi minne ni miongoni mwa walioambukizwa virusi hivyo.

Wagonjwa 219 waliokuwa wanapokea matibabu nyumbani wamepona na wnegine 14 waliokuwa hospitalini pia wakidhibitishwa hawana virusi hivyo na kufikisha idadi ya wlaiopona kuwa 26, 659.

Watu watatu zaidi wamefariki baada ya kuambukizwa virusi hivyo na kufikisha idadi ya waliofariki kuwa 731.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here