Francis Meja ameapishwa rasmi kuwa mwenyekiti mpya wa Tume ya Utumishi wa Umma (PSC) kuchukua nafasi iliyoachwa na balozi Anthony Muchiri.
Kuapishwa kwa Meja kumejiri siku chache baada ya rais William Ruto kumteua na bunge la kitaifa kumuidhinisha akitarajiwa kuhudumu kwa muhula wa miaka sita.
Akiongoza hafla ya kumwapisha iliyofanyika Jumatano tarehe 4 Machi katika majengo ya mahakama ya upeo jijini Nairobi, jaji mkuu Martha Koome aliirai tume hiyo kuzingatia uadilifu na maadili ya kikatiba katika uongozi wake.
‘‘Tume inabeba jukumu la kutekeleza kipengee cha 234 cha katiba ambacho kinasisitiza maadili ya kikatiba katika sekta ya utumishi wa umma, kuimarisha utendakazi wa kitasisi na kuendeleza ubora wa kitaaluma,’’ Alisema Koome.
Meja ambaye amehudumu katika sekta ya umma na binafsi kwa muda amekuwa mwanachama wa tume hiyo kuanzia mwezi januari mwaka 2025.
Kabla ya uteuzi wake Meja alikuwa mkrugenzi mkuu wa Mamlaka ya Kitaifa ya Uchukuzi na Usalama (NTSA)









