Gavana wa kaunti ya Trans-Nzoia George Natembeya amepata nafuu baada ya mahakama kumwondolea mashtaka ya uhalifu yaliyokuwa yakimkabili kutokana na ukiukaji wa katiba wakati wa kukamatwa kwake.
Katika uamuzi wake jaji wa mahakama ya Milimani Bahati Mwamuye alibaini kwamba Tume ya Maadili na Kukabili Ufisadi (EACC) ilikiuka sheria kwa kumnyima Natembeya fursa ya kuwasiliana na mawakili wake wakati wa kumkamata mwezi Mei 2025.
Mahakama vile vile iliamua kuwa njia ambayo wachunguzi katika kesi hiyo walivyopata taarifa za akaunti ya M-Pesa za gavana ilikuwa kinyume na sheria ikishikilia kuwa haikuafiki vigezo vya kikatiba.
Jaji Mwamuye zaidi aliamua kuwa taasisi ya kukabili kesi ya ufisadi dhidi ya Natembeya ilikosea heshima mchakato wa mahakama na kuzuia EACC pamoja na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP) kuendelea na mashtaka.
Kutokana na hilo mahakama iliamuru gavana Natembeya kulipwa shilingi milioni 2.5 kwa kukiukwa kwa haki zake za kikatiba.









