Aliyekuwa mbunge wa Changamwe na waziri msaidizi Ramadhan Seif Kajembe amefariki dunia akipokea matibabu katika hospitali ya Pandya, Mombasa.
Kajembe ameaga dunia chini ya majuma mawili baada ya mkewe kufariki kutokana na matatizo yanayoambatana na COVID19.
Mbunge huyo wa zamani hakupata fursa ya kuhudhuria mazishi ya mkewe Aziza Kajembe kwani alikuwa amelazwa hospitalini.
Mazishi ya mwendazake yatafanyika saa moja usiku wa leo Ijumaa katika makaburi ya familia ya Kajembe, eneo la Changamwe.
Kajembe aliwakilisha eneo bunge la Changamwe kwa mihula mitatu kuanzia mwaka 1997 hadi 2013.
Naibu rais William Ruto na kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga wametuma risala za rambi rambi kwa familia ya marehemu kufuatia kifo hicho.









