Baadhi ya maseneta wanapendekeza kuwe na mfumo ambapo kila mtu ataridhika katika kutanzua mjadala unaoendelea kuhusu ugavi wa mapato.
Maseneta hao akiwemo Kipchumba Murkomen wa Elgeyo Marakwet na Mutula Kilonzo Jr wa Makueni wamesema wanaunga mkono marekebisho yanayopendekezwa na maseneta Johnson Sakaja wa Nairobi na mwenzake wa Meru Mithika Linturi.
Yakijiri hayo
Tume ya uwiano na utangamano wa kitaifa (NCIC) imeelezea wasiwasi wake kuhusu kuingizwa siasa kwenye mjadala unaozingira mswada tata wa ugavi wa mapato.
Mwenyekiti wa tume hiyo askofu Samwel Kobia amewataka viongozi kuendeleza mjadala huo kwa njia komavu ili kuepuka kuwagawanya Wakenya kwa misingi ya kikabila.
Kuu kwenye taarifa hiyo, NCIC inawashauri wanasiasa kuepuka uchochezi kupitia kurushiana maneno wakati wa mjadala huo na badala yake walenge kuwaunganisha wananchi.