Naibu spika wa bunge la kitaifa Moses Cheboi anauguza majeraha katika hospitali moja baada ya kuhusika katika ajali ya Barabarani katika barabara kuu ya Molo kuelkea Mau-Summit Jana jioni ambapo mtu mmoja alifariki.
Inaarifiwa kuwa spika huyo ambaye ni mbunge wa Kuresoi kaskazini alikua akisafiria Gari lake aina ya Mercedes Benz ambapo aligongana ana kwa ana na pikipiki na kusababisha kifo cha mwendeshaji pikipiki hiyo.
Akidhibitisha ajali hiyo, kamanda wa polisi kaunti ya Nakuru Titus Kilonzi amesemaa mbunge huyo alikuwa akielekea maeneo ya Molo kabla kuhusika kwenye ajali hiyo.
Mwili wa marehemu ulipelekwa kwenye chumba cha maiti katika hospitali moja Nakuru uchunguzi zaidi ukiendelea.









