“Emuhaya iko mbele” – Utafiti

0

Mbunge wa Emauhaya Omboko Milemba ndiye anongoza kwa uwajibikaji kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni uliotolewa na kampuni ya Infotrack Harris.

Mkurugenzi mkuu wa Infotrack Angela Ambitho anasema Milemba ambaye pia ni mwenyekiti wa muungano wa kutwtea walimu wa shule za upili na vyuo vya kadri KUPPET ana asilimia 75.4 akifuatwa na mbunge wa Emurua Dikirr Johanna Ngeno ambaye ana asilimia 71.4.

Mbunge ambaye anaburura mkia kwa utendakazi kwa mujibu wa utafiti huo ni Abdi Koroputepo wa Isiolo Kusini ambaye ana asilimia 33 pekee akifautwa na Muturi Kigano wa Kangema ambaye ana asilimia 36.3.

Miongoni mwa wabunge wanawake, Naomi Shaban wa Taveta ndiye mwanamke bora zaidi kwa utendakazi akiwa na asilimia 61.6 akifuatwa kwa karibu na Edith Nyenze wa Kitui magharibi aliye na asilimia 58.4 kwa mujibu wa utafiti huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here