Maafa ya corona Kenya yafikia 700

0

Wakenya watatu ni miongoni mwa watu 53 waliokutwa na virusi vya corona baada ya kupima sampuli 1,107 katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe ambaye amesifia namna taifa limekabiliana na ugonjwa huo amesema hii inafikisha 38,168 idadi ya visa vya ugonjwa huo hapa nchini kufikia sasa.

Watu 60 wamepona na kufikisha idadi ya waliopona ugonjwa huo kuwa 24,681 huku idadi ya maafa ikiongezeka na kufikia 700 baada ya kufariki kwa wagonjwa 9 zaidi.

Msambao wa visa hivyo hamsini na attu ni kama ifwatavyo; Nairobi na Meru 11, Kiambu na Uasin Gishu 6, Nakuru 4, Kajiado 3, Garissa, Busia, Laikipia, na Machakos 2, Makueni, Embu, Kisumu na Kwale 1.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here